Kabla Hujanunua Simu Soma hii.

Mambo Muhimu ya kuzingatia kabla ya kununua simu.

MAMBO 10 YA KUZINGATIA KABLA UJANUNUA SIMU
1: BEI Kwanza ni lazima ujue una budget ya Shingapi ya kununua simu either ni laki 3 5 milioni na kuna wale wa “we taja simu kali achana na bei”. Baada ya kujua hilo 2: PROCESSOR Huu ndio ubongo wa simu mambo 
 
yote yanayofanyika kwenye simu upitia hapa. Ndiyo sehemu inayounganisha hardware na software kwenye simu, tunapaita SoC (System on Chip). Zimegawanyika katika makundi 3
▪️Entry level Chipset (150K-499K)
▪️Mid-Range Chipset (500K – 1.39m)
▪️Flagship Chipset (1.4m++)
 
Kuna kampuni 5 zinazofanya vizuri katika utengenezaji wa hizi Chipset (Processor)
▪️Apple (A Bionic) ▪️Snapdragon
▪️Huawei (Kirin)
▪️Samsung (Exynos)
▪️MediaTek (Dimensity & Helio) Kati ya hizo ni Samsung pekee mwenye uwezo wa kuziunda hizo Chipsets pekee yake
 
Kuna kampuni inaitwa TSMC ndiyo kiwanda chake kinatumika kuziunda za Apple, Huawei na Snapdragon na MediaTek pia kiwanda cha Samsung kinaziunda Exynos, Snapdragon na Google Tensor. Ni teknolojia kubwa sana haya makampuni yanafanya kupeleka Architecture ya Chipset zao.
 
A Bionic, Snapdragon na Kirin zinasifika sana kwa kuwa Chipset zilizokamilika zaidi pia Exynos na MediaTek baadhi. Yote kwa yote ni kukufanya ukiwa unatumia simu yako kila kitu ukione kipo vizuri. Kuna issue ya image processing, speeds n.k.
 
Tuje hapa mfano una budget ya laki 3 hapo kuna simu nyingi za makampuni tofauti tofauti na zimetumia processor za Snapdragon 680, MediaTek Helio G25, G33, F35, Exynos 855. Hapo simu yenye performance nzuri ni hiyo iliyotumia Snapdragon 680 🚀
 
Au mfano kwenye laki 7-8 unakutana na simu zenye Snapdragon 680, 720G, 732G, 778 5G, Exynos 1280, MediaTek G96 hapa yenye 778 5G ndiyo itakayokuwa na performance nzuri ikifuatiwa na Exynos 1280. Hakuna simu yenye processor kubwa ikawa na Camera ya hovyo.
 
3: SOFTWARE Nje ya iOS na Android kuna Android Skin au UI (User Interface) ni vyema hapa uchague simu itakayokuwa inakufanya uwe free zaidi, na isiyokuwa na Pop Ads (matangazo) Pia simu inayopokea software updates nyingi zaidi kwa simu za chini ya laki 5 huwa nyingi ni x 1 au 2
 
Pia kuna zile features za kipekee mtu anahitaji awe nazo kwenye simu na sio kila simu unaweza zikuta Mfano
▪️IR Blaster
▪️NFC
▪️Mult Apps
▪️Geisture sensors
▪️n.k
 
4: CAMERA Ubora wa Camera hautafsiriwi kwa wingi wa Megapixels, ubora wa Camera unatafsiriwa kwa simu kuwa na
▪️Camera sensor bora
▪️Software bora (IPS ndani ya Chipset)
▪️Lens Unakutana na simu ina 108MP inazidiwa na yenye 12MP.
 
Hapa kwenye camera kuna watu wa aina mbili
▪️Kuna ambaye anataka picha zenye muonekano mzuri
▪️Kuna ambaye anataka picha zenye details za kutosha na uhalisia. Utajuaje simu unayotaka kununua inapiga picha kwa viwango unavyotaka wewe?
 
Kama sehemu wanapokuuzia simu hawa sample za picha zilizopigwa na hiyo simu nenda Instagram search hashtag ya jina la hiyo simu utakutana na baadhi ya wasamaria kutokea hizo pande wamepost baadhi ya picha walizopiga kwa hiyo simu.
 
Pia picha haziwezi kuwa na ubora sawa kutokana na mazingira kutofautiana. Kwenye comparison ya simu ipi ina Camera kali muandaaji ndiye anayeamua mshindi awe nani. Mfano S22 Ultra unaweza iona picha nzuri kuliko iPhone 13 Pro Max na 13 Pro Max unaweza ona picha nzuri kuliko S22.
 
 
5: DISPLAY Simu zenye display bora siku zote huwa ni ghali, display zipo za aina tofauti kuna
▪️IPS LCD NA PLS
▪️OLED
▪️AMOLED
▪️Super AMOLED
▪️Fluid AMOLED
▪️Super Retina XDR OLED ▪️Dynamic AMOLED
 
All in All display nzuri zinaanzia kwenye AMOLED na simu kwenye simu moja moja kuanzia kwenye budget ya 500K 6: BATTERY Battery kuwa na 6000mAh sio kwamba ndio inaifanya simu itunze chaji muda mrefu kuliko yenye yenye 4500mAh huo ni ukubwa tuh. Simu kula chaji kunasababishwa
 
Na softwares & hardwares kwa pamoja ndivyo vinavyofanya simu unayoitumia itunze chaji kwa muda mrefu au mfupi, si ulishawahi sikia mtu baada ya kuupdate simu yake anajivunia kuw haili tena chaji au analalamika inakula haraka?
 
Mfano Oppo Reno 5 ina battery lenye 4310mAh ila inatunza chaji muda mrefu zaidi ya Redmi 9T yenye 6000mAh. Au iPhone 13 Pro Max yenye 4352mAh inatunza chaji muda mrefu kuliko Samsung S22 Ultra yenye 5000mAh.
 
Kuanzia 2020 mpaka sasa makampuni ya simu yamepiga hatua kubwa katika power management tofauti na zamani simu kila baada ya masaa manne inamiss kumbatio la charger. Pia kuna fast charging hapa kampuni kama Xiaomi na mengine kama Oppo, Oneplus, Vivo, Realme, iQOO, Infinix
 
Yanafanya vizuri sana. Kama Xiaomi Redmi Note 11 Pro+ 5G ina 120W HyperCharger inatumia tuh dakika 15 kufikisha 100%. Hii ni kukurahisishia muda. Kampuni nyingi zipo kwenye 18W-67W ni kuchaji simu ndani au nje ya lisaa limoja.
 
Kwa simu zote Original zinazofanya vizuri sokoni kwanzia 250K – 3.2m karibu ingia hapa ili uweze kutuma order yako sasa.
▪️Xiaomi (Redmi & Poco)
▪️Oppo (Oneplus & Realme)
▪️Samsung
▪️Infinix

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart
Scroll to Top